Wakazi - Barua Ya Wazi (MZALENDO)
Verse: 1
Dear Mr President, It's so humbly, nachukua fursa hii
Kuelezea ninayoyaona, kama kioo cha Jamii
Na pia kupendekeza mambo na mipango baadhi
As a citizen of the republic, and not Wakazi the artist
Kiuchumi tumekwama Mzee
Na tunahitaji, strategy ili hapa tu lipo tujikwamue aisee
I think Kidogo tuli stabilize in 2019
Ila tumerudishwa nyuma na hii Covid 19
Walale pema, walioangamia kwa Corona
Wengi kwa mamia, ila jitihada tumeona
Pongezi kwa Wizara, kwa mikakati ya hii homa
Ila changamoto za Afya nchini ni mziki, kama ngoma
Rule by iron fist, in some cases it's great
But could send a wrong message to insurbordinates
Waka overdo what they see from you, and emulate
Hoping kupandishwa vyeo, or simply for acknowledgment to get
They Create fear among people with scare tactics
Na kuwaminya wananchi, as if hawana haki
Wakati wanazo, tena kwa mujibu wa Katiba
It's their right, to express themselves yes and speak up
Ndugu speaker, TULIA acha wapinzani waongee
it's their JOB enforcin' accountability, do yours Mzee
Ndugu Rais, naongea na wewe ila pia na wananchi
Barua hii ya Wazi, is addressin' maswala nyeti ya nchi
Utata wa Swala la Muungano, kwa mfano
Marekebisho ya katiba
Siasa za maridhiano
Mahakama Huru, na tume huru ya uchaguzi
Pia kitaa wanataka arudishwe Assad wa Ukaguzi
Ukawa bado, struggle, ila penye nia pana njia
Sina hela, but for demokrasia, I go hard for Tanzania
So Leo hii, Tega sikio, nimeshaliza la mgambo
Ni mimi Mwananchi wa kawaida, Mzalendo
Verse: 2
Wanasema ukinywa pombe unaongea ukweli
Ila wasanii John Pombe hawamwambii ukweli
WanaMzunguka na kutaka Picha kama JK
Kumlewesha Sifa, hadi anahisi we are all okay
We are not, tuna shida kadha wa kadha
hatuzisemi, na tunang'ang'ana kuwa makada wa Chama
Wengine hata nyumbani hawajahama
Can't afford chumba na sebule, mitaa ya kijitonyama
Kila swala la sanaa linafanywa kisiasa
Wanaoumia sio mastaa wanaong'aa, ni sisi hasa
Ambao gari la mshahara hatujalinasa
Au pengine lilikuwa njiani linakuja, likapata pancha
Ni dhahiri, kwenye Mabenki hatukopesheki
Ujira mdogo so tunakosa mtaji wa kutupiga jeki
Hatuna mfuko wa Hifadhi wala Bima, hali haielezeki
Kwa kweli huu Muziki ni sawa na kazi feki
Sipendi ongelea utendaji wa Basata na Cosota
Ila Wasipowawezesha, wenye wataendela kusota
Tupo chini ya Wizara Tatu na bado sanaa inazorota
Kunahitajika mabadiliko, na sio tu mapromota
Tunataka mabadiliko na Uwazi, change and transparency
Commitment, Uzalendo na pia Uwajibikaji
Siasa ni msimamo, siasa ni itikadi
Siasa ilete viongozi, isitumike kama mtaji
Itumike kutumikia, Wakazi wa eneo fulani
Si tu kuweka ahadi, bali kutimiza ilani
Mi ni kiongozi tayari, nawakilisha kwa fani
Na siwezi sita, kuwakilisha Ukonga, nyumbani
Muda ukifika, ila kwa sasa nasambaza Upendo
Nakijipiga msasa, na kuyaziba mapengo
Kujenga msingi, utaosimamisha majengo Ki malengo
Ni mimi Mwananchi wa kawaida, Mzalendo