GLOBAL HABARI OCT 27: WALIOFARIKI KWA MAFURIKO TANGA WAFIKIA 14
Idadi ya vifo vya watu waliosombwa na mafuriko yaliyoikumba miji na vijiji vya Korogwe na Handeni Mkoani Tanga kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha imeongezeka na kufikia 14 hadi leo jumapili asubuhi.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tanga,Edward Bukombe ni kwamba jana jumamosi iliopolewa miili 11 wakati leo imeonekana miili ya watu watatu
Athari hiyo imetokea mara baada ya mvua kubwa zinazoendelea kunyesha licha ya daraja hilo kukatika pia daraja la mandera ikiwa ni barabara kuu ya segera lililopo korogwe kujaa na kusababisha wananchi kushindwa kuendelea na shughuli zao.
Naibu waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano alifika eneo la tukio na kusema kuwa wao kama wizara kwa kushirikiana na serekali ya mkoa wamejipanga hali inarudi kama ilivyokuwa hapo awali ili wananchi wasiendelee kupata mateso na kuhakikisha wanaendelea na shughuli zao kwani kutokuendelea kwa safari kwa magari hayo kiuchumi ni hasara kubwa.
Kwa upande wake wake meneja wa Tanroad mkoa wa Tanga Alfredi Ndumbalo amesema watahakikisha wanafanya kazi usiku na mchana hivyo wanasubiri mvua zikatike ili mawasiliano yarudi kama ilivyokuwa.
Oktoba kumi na tatu mvua ilisababisha kukata mawasiliano kwa barabara inayotoka dar es slaam kwenda mkoani tanga na kusababisha msongamano wa magari katika eneo hilo baada ya siku kumi na tatu mvua hiyo ikaleta madhara Zaidi kwa kuharibu miundo mbinu na kupelekea watu saba kupoteza maisha.
#GLOBALHABARI
YALIYOMO GLOBAL TV ONLINE (+255 657 955825 au +255 784 888982)
---------------------------------------------------------------------------------------
HABARI MPYA DAILY:
https://www.youtube.com/playlist?list...
HISTORIA ZA VIONGOZI ZA KUSISIMUA:
https://www.youtube.com/playlist?list...
GLOBAL RADIO TV:
https://www.youtube.com/playlist?list...
EXCLUSIVE INTERVIEWS:
https://www.youtube.com/playlist?li