Home » News & Politics » SIMANZI! Agnes Masogange aagwa kwa vilio, Rammy Galis azimia!

SIMANZI! Agnes Masogange aagwa kwa vilio, Rammy Galis azimia!

Written By Samfrod TV on Monday, Apr 23, 2018 | 10:18 AM

 
Ni katika kuhitimisha safari ya Mwisho ya Marehemu Agnes ambaye alikuwa ni Video Vixen aliyejizolea umaarufu mkubwa kupitia kuonekana katika Video za wasanii na hatimaye kuingia katika tasnia ya Filamu kupitia Filamu aliyoigiza na Msanii mwenzie Rammy Galis ambaye pia alitokea kuwa na mahusiano nae yaliyodumu kwa Miezi 11. Kwa upande wa Viongozi wa kiserikali waliongozwa na Mkuu wa Wilaya Mhe. Ali Hapi na viongozi wengine wa Kisiasa pamoja na wasemaji wa vilabu akiwemo Haji S. Manara wa Simba Sports Club. Hakika wasanii na watu mbalimbali waliomfahamu na kuishi nae kwa namna moja ama nyingine alitikea kuzigusa nyoyo zao nao wakajitokeza katika kutoa salamu zao zao za mwisho akiwemo mwanamuziki Diamond Platnumz, Ali Kiba, Chegge, Mrisho Mpoto, Shilole, Dogo Janja na wengine wengi. Katika Bongo Movies walijitokeza wengi; Irene Uwoya, Jackline Wolper, Irene Paul, Richie Rich, Steve Nyerere, Dr. Cheni na wengine wengi. Na Mavideo Vixen wenzie alikuwepo mwanadada Hamisa Mobetto, Official Lynn, Jini Kisirani, Isha Madonna, Agnes na wengine wengi.