Home » News & Politics » KESI YA WEMA SEPETU BADO KIZUNGUMKUTI

KESI YA WEMA SEPETU BADO KIZUNGUMKUTI

Written By Mwananchi Digital on Wednesday, Oct 04, 2017 | 07:48 AM

 
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imekwama kutoa uamuzi wa kupokea ama kutopokea kielelezo cha hati ya ukamataji nyumbani kwa Wema Sepetu katokana na Hakimu kutomaliza kuandaa uamuzi huo. Uamuzi huo ulitarajiwa kutolewa leo October 4, 2017 na Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba lakini amesema bado hajamaliza kuandaa uamuzi huo ambapo ameahirisha kesi hiyo hadi November 1,2017. Mbali ya Wema washtakiwa wengine ni Angelina Msigwa na Matrida Abbas ambapo wanakabiliwa na mashtaka mawili ya kukutwa na kiwango kidogo cha dawa za kulevya na kutumia dawa za kulevya