Home » People & Blogs » Baba wa mtoto aliyeokoa maisha ya watu 9 asimulia ushujaa wa mtoto wake ulivyomfikisha Dar

Baba wa mtoto aliyeokoa maisha ya watu 9 asimulia ushujaa wa mtoto wake ulivyomfikisha Dar

Written By Dar24 Media on Saturday, May 27, 2017 | 05:15 AM

 
Baada ya mtoto Tisekwa Gamungu kuwaokoa wanafunzi wenzake tisa kuzama ziwa victori kufuatia mtumbwi waliokuwa wakiutumia kwaajili ya kuvuka kupinduka na kuzama, Baba wa mtoto huyo Gamungu Pesambili ameelezea tukio hilo kuwa ni la ujasiri wa hali ya juu. Gamungu amesema kuwa katika maisha yake alikuwa hajawahi kufikilia wala kujua kwamba mwanae anauwezo mkubwa wa kuogelea kiasi cha kuweza kuwaokoa wanafunzi wenzie tisa.. Aidha, kufuatia tukio hilo Gamungu amewaasa wazazi wenzie kuwasikiliza watoto kile ambacho wanakipenda katika maisha hivyo kuwawezesha kwakuwa watakifanyia kazi vizuri. "Nawaomba wazazi wenzangu tuwasikilize watoto wanachotaka kukifanya katika maisha yao tuwange mkono ili kuweza kuwawezesha kufikia malengo yao,"amesema Gamungu. -- Dar24 ni chanzo namba moja cha habari kwa watanzania mahali popote walipo duniani. Kwa habari za uhakika kutoka nyanja mbali mbali tembelea www.dar24.com #Dar24 #Dar24Media