Home » News & Politics » Dereva wa Ajali ya Narok Ashtakiwa

Dereva wa Ajali ya Narok Ashtakiwa

Written By Citizen TV Kenya on Thursday, Sep 05, 2013 | 01:45 AM

 
Steve Mutia dereva wa basi lililosababisha ajali ya Ntulele na kupoteza maisha ya abiria 42 alifikishwa mahakamani hii leo baada ya kujisalimisha kwa polisi hapo jana jioni. Mutia anakabiliwa na mashtaka arobaini na mawili na makosa mengine ya trafiki ambayo aliyakanusha mbele ya hakimu mkaazi Bi Zainab Abdul huku kila abiria aliyeaga akiandikishwa kama mlalamishi kibinafsi na kama anavyotuarifu Pheona Kengah kesi hiyo itasikizwa tarehe kumi na nane mwezi novemba mwaka huu.